Southampton wavuta jembe la Liverpool Takumi Minamino

Klabu ya Southampton imefanya usajili wa mshambuliaji wa Liverpool Takumi Minamino kwa mkopo wa mpaka mwishoni mwa msimu huu. Watakatifu Southampton wamemsajili mchezaji huyo raia wa Japan ambaye amekosa nafasi ya kutosha ndani ya Majogoo wa Jiji la Merseyside.

Anaenda Saints kuchukua nafasi ya Shane Long, ambaye ameenda kujiunga na AFC Bournemouth inayoshiriki Ligi daraja la kwanza nchini England. Minamino, 26, alijiunga na Liverpool kwa ada ya pauni milioni 7.25 kutokea Red Bull Salzburg Januari ya mwaka 2020. Amecheza mechi nne tu tangia alivyoingia Anfield.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares