Southgate mkataba mpya England

Kocha wa timu ya taifa ya England Gareth Southgate ameongeza kandarasi mpya ya kuendelea kukitumikia kikosi hicho, mkataba utakaodumu mpaka Disemba 2024.

Southgate, ambaye mkataba wake wa awali ulikuwa unamalizika mwishoni mwa mwaka 2022 baada ya fainali za Kombe la Dunia Qatar 2022, baada ya kuingia kwa mara ya kwanza Novemba 2016 baada ya Sam Alladyce kuwekwa kando.

Miongoni mwa mafanikio makubwa ambayo katika kipindi chake, Southgate alikiongoza kikosi cha Three Lions kufika hatua ya fainali ya Euro 2020, mafanikio ambayo ni makubwa kwa zaidi ya miaka 55 kwa timu ya taifa.

“Inabakia kuwa bahati ya kipekee, kuongoza hii timu. Tuna nafasi kubwa mbele yetu ambayo kila mmoja anaitazama”, alisema Southgate.

Author: Asifiwe Mbembela

Share With Your Friends