Spurs ya Mourinho yatimuliwa na RB Leipzig

Klabu ya Tottenham Hotspurs ya kocha Jose Mourinho imeyaaga rasmi michuano ya UEFA Champions League msimu wa 2019/20 kwa kuondolewa na RB Leipzig, licha ya msimu uliopita kufika hadi hatua ya fainali.

Mourinho na vijana wake walikuwa ugenini Ujerumani lakini walienda kutafuta ushindi kwa kuwa mchezo wa kwanza nyumbani kwao London walipoteza mchezo huo kwa kufungwa goli 1-0.

Mchuano wa marudiano umekuwa mbaya zaidi kwa Mourinho kwa kujikuta akipoteza mchezo wa pili kwa kufungwa kwa magoli 3-0, magoli ya RB Leizig yakifungwa na Marcel Sabtzer aliyefunga mawili dakika ya 10 na 21 na mwisho likafungwa na Emil Forsberg dakika ya 87.

Katika matokeo mengine ya keo, Atalanta wamejikatia tiketi baada ya ushindi wa 4 – 3 dhidi ya Valencia

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends