Staa wa Liverpool Mane alipeleka Senegal AFCON 2022

Staa wa Liverpool Sadio Mane ameipeleka timu yake ya taifa ya Senegal katika fainali za Kombe la Mataifa barani Afrika AFCON 2022 baada ya kufunga goli pekee na la ushindi dhidi ya Guinea-Bissau.

Kwenye mchezo huo, Mane aliweka mpira nyavuni dakika ya 82 baada ya Jorge Nogueira kutupwa nje ya uwanja kwa kadi nyekundu kwa upande wa Guinea-Bissau.

Senegal, ambao wanashikilia nafasi ya kwanza barani Afrika kwenye viwango vya Fifa wanakuwa taifa la kwanza kufuzu kushiriki michuano hiyo mikubwa ngazi ya taifa baada ya Cameroon ambao wanafuzu moja kwa moja kutokana na kuwa waandaaji wa mashindano hayo.

Wamevuna alama 12 kwenye mechi nne kundi I huku zikiwa zimesalia mechi mbili. Mane alifunga kwa penati katika ushindi wa Senegal 2-0 dhidi ya Guinea-Bissau siku ya Jumatano.

Fainali za mwaka 2021 zilihairishwa kutokana na janga la virusi vya Corona na kusogezwa mbele mpaka Januari ya mwaka 2022 na Shirikisho la kandanda barabi Afrika CAF.

Author: Bruce Amani