Stars kibaruani kuikabili Tunisia kufuzu AFCON 2021

Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ itakuwa na kibarua cha kumenyana na timu ya Taifa ya Tunisia katika mchezo utakaochezwa Uwanja wa Stade Olympique de Rades Marchi 27 mwaka huu.

Mchezo huo ni maalumu kwa ajili ya Taifa Stars kufuzu michuano ya Afcon kwa mwaka 2021 ambapo mpaka sasa Tanzania imecheza michezo miwili mmoja ikashinda (Equatorial Guinnea) na mwengine kupoteza (Libya) katika kundi J.

Kwenye mchezo huo waamuzi watatoka Angola ambao ni Helder Martins Rodrigues De Carvalho-Katikati -Jerson Emiliano Dos Santos-Msaidizi 1, Ivanildo Meirelles De O Sache Lopes-Msaidizi 2, Joao Amado Muanda Goma-Akiba.

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Etienne Ndayiragije amesema kuwa ana matumaini ya kupata matokeo chanya kwenye mchezo huo. Timu mbili za juu kila kundi zinafuzu moja kwa moja kwenda Kombe la Mataifa Afrika AFCON 2021 nchini Cameroon.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends