Sterling mguu pande Manchester City, Madrid yahusika

Winga wa Manchester City Raheem Sterling amesema Real Madrid ni klabu bora lakini amesisitiza kuwa anafuraha kubwa kuendelea kusalia Manchester City.

Sterling, 25, amekuwa alihusishwa kujiunga na Real Madrid tangu City ilipokumbwa na kifungo cha kutoshiriki mashindano ya Ulaya kwa misimu miwili sawa na miaka miwili.

“Saizi niko City na nina furaha kubwa kuwa hapa. Lakini nasema kuwa Real Madrid ni klabu kubwa na bora sana,” Sterling alisema hayo alipozungumza na Gazeti la AS la Hispania.

“Unapoitaza jezi nyeupe unajua kabisa inasimama kuwakilisha timu hatari.” Aliongeza Sterling ambaye amekuwa nguzo ya Manchester City siku za usoni chini ya Pep.

City inategemea kusafiri kwenda Madrid kucheza na mabingwa mara nyingi zaidi wa Uefa(13) hatua ya 16 ya ligi ya Mabingwa raundi ya kwanza kabla ya kurudiana Marchi 17.

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema hana maamuzi yoyote juu ya kile atakachokiamua Raheem Sterling kwani masuala yote yapo chini yake.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends