Suárez aficikisha mechi 200 La Liga, wakati Atletico ikishinda 3 – 1 Elche

74

Atletico Madrid wameenda kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu nchini Hispania wakiwa na alama tatu baada ya kushinda dhidi ya a Elche wakiwa bado wana mechi mbili mkononi.

Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool na Barcelona Luis Suarez alitupia bao akimalizia pasi ya beki wa kulia Kieran Trippier. Yannick Carrasco alimpa usaidizi mwingine Suárez akatupia bao la pili kabla ya Lucas Boyle kufunga goli kwa upande Elche.

Jioni mchezaji aliyetokea benchi Diego Costa alifunga goli kwa njia ya penati na kufanya mchezo huo kumalizika kwa goli 3-1.

Ushindi huo unaifanya Atletico kuwa mbele ya Real Madrid, Real Sociedad, ambao wana alama pungufu na michezo wakati wakiipita Barcelona kwa alama tisa.

Suarez, ametimiza mechi yake ya 200 ndani ya La Liga ambapo sasa, amefunga goli saba katika mechi tisa ndani ya Atletico Madrid.

Author: Asifiwe Mbembela