Tabasamu kwa Namungo FC, yala dili nono kwa kuingia kandarasi ya mwaka mmoja na Sportpesa

Namungo FC inayoshiriki michuano ya Ligi Kuu nchini Tanzania na Kombe la Shirikisho barani Afrika imeingia kandarasi ya mwaka mmoja na Kampuni ya michezo ya kubashiri Tanzania, SportPesa wenye thamani ya shilingi milioni 120. Mkurugenzi wa SportPesa Tanzania, Abbas Tarimba amesema kuwa wameamua kufanya hivyo kutokana na kuridhishwa na mwenendo wa timu hiyo inayoshiriki Kombe la Shirikisho Afrika.”Tumeridhishwa na mwenendo wa Namungo FC kwenye Kombe la Shirikisho Afrika pamoja na namna ambavyo wanapambana kuweza kupeperusha bendera ya Tanzania. “Tunaamini kwamba huu ni mwanzo na ina nafasi ya kufanya vizuri kimataifa hivyo tunawatakia kila la kheri na tutazidi kuwa pamoja katika sekta ya michezo,”.

Mwenyekiti wa Namungo FC,Hassan Zidadu amesema kuwa wanashukuru kwa udhamini huo na wanaamini kwamba utawapa nguvu ya kupamba zaidi kitaifa na kimataifa. “Tunashukuru kwa ajili ya udhamini wa ambao wameweza kufanya kwetu na tunaahidi kupambana zaidi kwa ajili ya mechi zetu za kitaifa na kimataifa pia.

Unakuwa ni mkataba wa pili baada ya ule wa awali kumalizika.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares