Taifa Stars hoi kwa Algeria

45

Taifa la Algeria limefanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano ya Kimataifa Afrika Afcon kwa staili yake baada ya kushinda michezo yote na kujikusanyia alama tisa huku ikiinyuka Tanzania goli 3-0 mchezo uliofanyika leo Julai Mosi.

Algeria ikiwa ina uhakika wa kusonga mbele iliwapumzisha zaidi ya wachezaji wanne walioanza mchezo ulipoita akiwemo Riyad Mahrez wa Manchester City na ikafanikiwa kupata goli la kwanza kupitia kwa Islam Slimani anayekipiga Fernabache kwa mkopo kabla ya goli mbili za haraka za winga wa Napoli ya Italia Adam Ounas.

Mabadiliko kadhaa kutoka kwa kocha wa Tanzania Emmanuel Amunike hayakufua dafu katika kukiweka sawa kikosi hicho kuepuka kipigo hicho, huku kikiwa kipigo cha tatu mfululizo kwenye mashindano ya Afcon 2019 baada ya Senegal na Kenya.

Matokeo hayo yanifanya Algeria kufuzu hatua ya 16 bora sambamba na Senegal huku Kenya ikisubiri nafasi ya tatu bora kusonga mbele kwenye michuano hiyo wakati Tanzania ikipewa mkono wa kwaheri.

Author: Bruce Amani