Taifa Stars watua Misri tayari kwa kivumbi cha Afcon

Zimesalia siku 12 kuanza mashindano ya soka, kuwania taji la mataifa ya barani Afrika.

Michuano hii itaanza tarehe 21 mwezi huu nchini Misri, na kwa mara ya kwanza mataifa 24 yatashiriki.

Timu ya taifa ya Tanzania, imekuwa ya kwanza kuwasili nchini Misri, baada ya kocha Emmanuel Amunike kuondoka na kikosi cha wachezaji 30 kuanza maandalizi wakiwa huko Misri.

Harambee Strs ya Kenya ipo nchini Uaransa kwa maandalizi yao, huku Uganda ikiwa Duba.

Burundi ambayo imefuzu kwa mara ya kwanza katika mashindano haya, nayo ipo huko Qatar kwa maandalizi zaidi.

Leopard ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambayo ipo nchini Uhispania kwa maandalizi yake, na kocha Florient Ibenge amesema kuwa wachezaji wake wanafanya bidii ili kuwa katika kikosi cha mwisho.

Kumekuwa na taarifa kuwa mshambuliaji wa DRC, Yannick Yala Bolasie ana jereha na atakosa fainali hii, lakini yupo na wachezaji wenzake huko nchini Uhispania,

Bolasie, anachezea klabu ya Anderlecht kutoka nchini Ujerumani, anakocheza kwa mkopo kutoka kwa klabu ya Everton.

Makala haya ya 32 ya AFCON, itachezwa katika viwanja sita,ule wa Kimataifa wa Cairo, Juni 30, Al Salam, Alexandria, Suez na Ismailia.

Author: Bruce Amani