Taifa Stars yafufua matumaini kuelekea Cameroon

299

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars imeamusha matumaini mapya kwa Watanzania ya kufuzu fainali za AFCON mwakani nchini Cameroon baada ya kuibuka na ushindi wa goli 2-0 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam maarufu kama Mkapa Stadium.

Ilikuwa ni dakika ya 29 ambapo nyota wa kimataifa wa Tanzania Saimon Msuva anayecheza katika klabu ya Diffa Al Jadida alifunga goli baada ya kazi kubwa iliyofanywa na mashambulaiji Mbwana Ally Samatta kwa kuwatoka mabeki wa Cape Verde. Hii ni baada ya dakika chache Samatta kukosa penati.
Katika kipindi cha pili ilikuwa ni dakika ya 58 Mbwana Samatta aliifungia Tanzania na kusawazisha makossa ya kukosa penalti baada ya pasi murua ya Mudathiri Yahya kwenye Boksi la Cape Verde.
Mchezo ulikuwa wa kasi kwa ujumla ambapo ilikuwa piga nikupige huku Tanzania wakitumia nafasi walizozipata kushinda na kutumia faida ya uwanja wa Nyumbani.

Katika mchezo huu Tanzania ilianza na kikosi hiki 1. Aishi Manula, 2.Shomari Kapombe, 3. Abdi Banda, 4. Agris Morris, 5. Kelvin Yondani, 6. Erasto Nyoni, 7.Himid Mao, 8.Mudathri Yahya, 9.Mbwana Samatta, 10. Saimon Msuva 11. Gadiel Michael.

Sasa Tanzania imepanda mpaka nafasi ya pili kwa alama 5, Uganda nafasi ya kwanza na alama 7 huku jioni ya leo inacheza mchezo dhidi ya Lesotho, timu ya mwisho ni Lesotho yenye alama 1.
Endapo Tanzania itafanikiwa kufuzu kwenda Cameroon itakuwa mara ya pili tangu mwaka 1980 ilipofanya hivyo ikiwa nchini Zambia.

Author: Bruce Amani