Tanzania hoi mbele ya Kenya katika dabi ya majirani

61

Timu ya taifa ya Tanzania “Taifa Stars” inaungana na Burundi kuondoshwa kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika AFCON 2019 baada ya kukubali kipigo kutoka kwa majirani zao Kenya “Harambee Stars” mtanange uliofanyika Alhamisi Juni 28.

Taifa Stars ikiwa chini ya nahodha anayekipiga katika klabu ya Genk ya Ubeligiji imeshindwa kufurukuta mbele ya Harambee Stars iliyo chini ya nahodha Victor Wanyama mchezaji wa Tottenham Hotspurs.

Licha ya kutangulia kwa goli la mapema la Saimon Msuva wa Tanzania haikuchukua muda mrefu goli hilo kusawazishwa kupitia mshambuliaji Michael Olunga. Hata hivyo haikuchukua muda mrefu kabla ya Mbwana Samatta kufunga bao la pili na kuiweka Tanzania kifua mbele 2-1 katika kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo Kenya walipata bao la kusawazisha kupitia mchezaji Johanna Omolo kabla ya Michael Olunga kufunga kazi na bao la tatu. Mbali na matukio ya ndani ya uwanja, mchezo huo ulibeba hisisa za Wanamshariki kutokana na kila mmoja kutumia mbinu yake kuleta hamasa kwa timu husika. Tanzania iliwapeleka Wabunge kabla ya Mkuu wa Mkoa Paul Makonda ambaye pia ni Mwenyekiti wa hamasa haijafua dafu juhudi hizo kutokana na matokeo ya leo.

Upande wa Kenya walitembelewa na mchezaji wao wa zamani McDonald Mariga ambaye matunda yake yameonekana kutokana na matokeo yao. Kenya imeendeleza ubabe dhidi ya Tanzania  kwani unakuwa ushindi wa nne katika michezo 5 waliocheza kwenye mashindano yote.

Author: Bruce Amani