Tanzania, Kenya, Uganda Kuandaa Kombe la AFCON 2027

171

Mataifa matatu jirani yanayounda Jumuiya ya Afrika Mashariki yameanza mchakato wa kuomba kuandaa kwa pamoja mashindano ya Kombe la Mataifa Bingwa Afrika AFCON 2027.

Taarifa ya kuanza mchakato huo zimesemwa na Waziri wa Michezo wa Kenya Ababu Namwamba ambaye amesema wameshawasilisha maombi rasmi kwa pamoja huku kushindwa kwa taifa la Namibia na Botswana kukiongeza nguvu ya kushinda.

“Tunakusudia kuandaa Afcon 2027 kwa pamoja na taifa la Tanzania na Uganda. Ninayo furaha kwamba mchakato huo unaenda vizuri”, alisema Ababu Namwamba. “Tunapanga kuyaleta mashindano hayo Afrika Mashariki “.

Author: Asifiwe Mbembela