Tanzania kuchuana na Burundi fainali ya CECAFA U-23 Ethiopia

Timu ya Taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 23 baada ya kufuzu kucheza fainali ya Cecafa U-23 Leo Ijumaa Julai 30 itamenyana vikali na taifa la Burundi ambapo kuelekea mtanange huo nahodha wa kikosi hicho Mwenda ajinasibu kufanya vizuri.

Tanzania ilipata nafasi ya kucheza fainali baada ya kuifunga Sudan Kusini bao 1-0 wakati Burundi ikiichapa Kenya kwa changamoto ya mikwaju ya penati 4-2 siku mbili zilizopita.
Nahodha wa kikosi cha Tanzania ambaye pia ni mchezaji wa Kinondoni Municipal Council (KMC) amesema kuwa wanamatumaini ya kufanya vizuri.
Tanzania imetinga hatua ya fainali mara baada ya kuifunga timu ya taifa ya Sudan Kusini kwa bao 1-0 huku Burundi wao wakiwatoa timu ya Kenya kwa mikwaju ya penati 4-2, mara baada ya timu hizo kutoka sare katika dakika 90.
“Tumedhamiria kuwa mabingwa wa michuano hii, tumefika fainali na tuna malengo ya kuwa mabingwa, kuhusu kurudi na kombe nyumbani pia tunatarajia kuona hilo likitokea, tunaomba maombi kwa watanzania wote.”amesema nahodha huyo.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares