Tanzania kupepetana na Burundi safari ya Qatar 2022

Timu ya taifa ya Tanzania “Taifa Stars” imepangwa kucheza na Intamba M’rugamba Burundi katika mchezo wa hatua ya awali kuingia kwenye makundi yatakayotumika kufuzu kucheza Kombe la Dunia Qatar 2022 mwezi Septemba.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika CAF lililo na makao yake Cairo Misri leo Jumatatu Julai 29 limepanga mechi za awali zitakazochezwa mechi mbili za nyumbani na ugenini huku timu itakayoshinda itafuzu hatua ya makundi ya timu tano kila kundi.
Katika droo ya iliyopangwa leo imehusisha timu 24 zilizochini kiviwango vya ubora vya FIFA mwezi Julai.
Timu 6 zilizo shiriki mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika Afcon 2019 zitaanzia hatua ya awali kutokana na kuzorota kwenye viwango vya FIFA ambavyo hutolewa kila mwezi Tanzania, Burundi, Angola ni miongoni mwa hizo.
Kwa ratiba inavyoonyesha ni kuwa Burundi itaanzia nyumbani kwa kuikalibisha Tanzania kabla ya kusafiri kuifuata Tanzania katika mchezo wa mkondo wa pili.
Droo nzima ya kufuzu Kombe la Dunia 2022 Qatar hatua za mwanzo/awali Afrika.
Ethiopia vs Lesotho
Somalia vs Zimbabwe
Eritrea vs Namibia
Burundi vs Tanzania
Djibouti vs Eswatini
Botswana vs Malawi
The Gambia vs Angola
Liberia vs Sierra Leone
Mauritius vs Mozambique
Sao Tome e Principe vs Guinea-Bissau
South Sudan vs Equatorial Guinea
Comoros vs Togo
Chad vs Sudan
Seychelles vs Rwanda.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends