Tanzania U-23 yaichapa Congo Cecafa

Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 23 imeanza vyema michuano ya Cecafa baada ya kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika mchezo wa Kundi A uliopigwa Jumanne Julai 21 dimba la Bahir Dar nchini Ethiopia.

 

Bao pekee katika mchezo huo limewekwa kimiani na mshambuliaji wa Namungo Fc, Relliant Lusajo dakika ya 66 ya mchezo wao huo wa kwanza wa michuano hiyo, ukiwa ushindi wa kwanza kwa Tanzania.

 

Kikosi hicho kinachonolewa na kocha Kim Poulsen kinaingia kambini tena huko huko Ethiopia kujiandaa na mchezo wa mwisho dhidi ya Uganda.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares