Tanzania warejea nchini baada ya kubeba Cecafa U-23

140

Baada ya kushinda ubingwa wa Kombe la Cecafa U-23, timu ya taifa ya Tanzania imewasili nchini Leo Jumapili Agosti Mosi kutokea Ethiopia ilikokuwa inashiriki michuano ya Cecafa na kubeba ubingwa mbele ya Burundi

Tanzania ilishinda kwa penati 6-5 mbele ya Burundi baada ya dakika 90 kukamilika matokeo yakiwa tasa.

Wakiwa uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF), Wallace Karia amesema kuwa ni jambo la furaha kwa ushindi waliopata.

Mbali na uongozi wa TFF, mashabiki pia walijitokeza kwa ajili ya kuwapokea wachezaji hao ambao wameweza kuipeperusha vema bendera ya Tanzania.

Wakiwa na ngoma zao mashabiki walipata pia muda wa kucheza na wachezaji wa U-23 pamoja na kupiga picha na kombe hilo nje ya uwanja kwa muda.

Author: Asifiwe Mbembela