Tanzania yaiondoa Kenya kwenye safari ya Chan

231
Timu ya taifa ya Tanzania “Taifa Stars” imesonga mbele hatua moja ya michuano ya kufuzu kucheza mashindano ya Chan baada ya kuifunga Kenya Harambee Stars nchini kwao Nairobi kwa penati 4-1 baada ya dakika za kawaida ndani ya uwanja wa Kasarani kumalizika kwa suluhu tasa.
Mchezo wa Jumapili umekuwa wa mkondo wa pili baada ya ule wa kwanza kufanyika Tanzania wiki moja lilopita na mpira kumalizika kwa suluhu ya 0-0.
Aidha, matokeo ya ushindi kwenye kipute cha leo imekuwa kama kisasi kwa Kenya ambao waliifunga Tanzania katika mashindano ya Kimataifa Afrika kwa maana ya AFCON 2019 Misri kwa goli 3-2.
Shujaa wa mchezo huo alikuwa ni Juma Kaseja Juma ambaye ameokoa michomo miwili ya penati kabla ya Erasto Nyoni, Paul Godfrey, Gadiel Michael na Salim Aiyee kutupia mpira nyavuni kwa maana ya kufunga na kuipendezesha Tanzania ugenini.
Baada ya mtanange wa leo sasa, Taifa Stars itacheza na Sudan katika hatua ya pili ya kutafuta nafasi ya kufuzu michuano ya Chan ambayo huusisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani kwa nchi husika.
Mchezo mwingine uliopigwa leo ni:-
Afrika Kusini 0-3 Lesotho.

Author: Bruce Amani