Tanzania yatupwa nje na Namibia kufuzu AFCON

Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania, Twiga Stars imeondoshwa nje mbio za kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuchapwa 3-2 na Namibia leo Octoba 23, Uwanja wa Dobsonville Jijini Johannesburg, Afrika Kusini.

Namibia imepata magoli yake kupitia kwa kiungo mshambuliaji wa Sevilla ya Hispania, Zenatha Goeieman Coleman yote matatu, wakati ya Twiga Stars yamefungwa na kiungo mshambuliaji wa Chabab Atlas Khenifra ya Morocco Mwanahamisi Omary Shaluwa ’Gaucho’ na mshambuliaji wa Simba Queens, Opa Clement Sanga.

Twiga Stars inatolewa kwa jumla ya mabao 5-3 kufuatia kufungwa goli 2-1 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam Jumatano.

Author: Asifiwe Mbembela

Share With Your Friends