Tarehe za michuano ya fainali za AFCON 2019 zabadilishwa

Shirikisho la soka barani Afrika wiki hii limetangaza mabadiliko ya kuanza kwa michuano ya fainali za kuwania taji la bara Afrika kutoka kutoka tarehe 15 mwezi Juni hadi Julai 13.

Michuano hii itaanza kuchezwa arehe 21 mwezi Juni na kumalizika tarehe 19 mwezi Julai nchini Misri.

CAF imefanya mabadiliko haya ili kuwapa nafasi wachezaji wa Kiislamu kupumzika baada ya kumalizika kwa mwezi Mtukufu wa Ramadhani, na mabadiliko haya yalifanyika baada ya maombi kutoka kwa Morocco, Tunisia na Algeria.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends