Tathmini ya wachezaji wa Yanga katika dabi ya Kariakoo

Mtanange wa Simba dhidi ya Yanga umekamilika kwa sare ya goli 2-2 baada ya kandanda safi kutoka kwa timu zote mbili.

Tamati hiyo inatoa fursa ya kutoa tathimini ya dakika 90 kwa wachezaji wa timi zote mbili na kutoa alama za kila mchezaji kulingana na uwezo aliouonyesha katika mchezo huo.

Tuanze na Yanga 

 1. Farouk Shikalo

Bila shaka ushindi wa Yanga leo umechagizwa na nyanda huyu kuwa kwenye milingoti miwili, katika kipindi cha kwanza aliokoa michomo kadhaa kutoka kwa Kagere sambamba na Francis Kahata.

Anapata alama 7.

 1. Juma Abdul

Siku za karibuni hana namba ya kudumu lakini alikuwa mhimili mkubwa katika mtanange huk bila shaka uzoefu umemsaidia. Hakuwezi kumzuia vyema Kahata na Mohammed Hussein kutoleta hatari hakufanya hivyo, hata krosi zake hazikuwa na hatari kama siku zote.

Anapata alama 5.

 1. Adeyum Ahmed

Kama mlinzi mpya kikosini hakuonyesha makeke makubwa licha ya kuliweka lango la Yanga salama.

Anapata alama 5.

 1. Ally Sonso

Hana uzoefu na Kariakoo Dabi lakini ni miongoni mwa wachezaji walionyesha ubora mkubwa sana, ameokoa mipira ya juu na ya chini pia alikuwa mwiba kwa Kagere na Chama Clatous.

Anapata alama 7

 1. Kelvin Yondani

Kama ilivyo kwa Sonso Hali kadhalika alikuwa mchezaji muhimu licha ya maamuzi yake kuigharimu timu kwa kumwangusha Kagere ndani ya 18.

Anapata alama 6.

 1. Abdulaziz Makame

Ameshindwa kuonyesha uwezo alionao kabisa. Alishindwa kupiga pasi sahihi wala hata uimara wake ulipo wa kurusha mipira hakufanya hivyo. Unaweza ukasema mchezo ulimzidi ukumbwa.

Anapata alama 4.

 1. Mohamed Issa Banka

Alikuwa hatumiki kwenye michezo ya usoni lakini ameibukia ndani ya mtanange wa watani wa jadi. Licha ya kufunga goli la pili hakuonyesha makeke.

Anapata alama 6.

 1. Papy Tshishimbi

Bila shaka kungekuwa na vifaa vya kuhesabu umbali ambao wachezaji wamekimbia uwanjani nchini, Tshishimbi angehusika, ametumika maeneo yote ya kiungo kuanzia mshambuliaji na hata ulinzi baada ya Makame kutoka.

Anapata alama 7.

 1. Ditram Nchimbi

Sio yule Ditram wa Njombe Mji na wala sio yule wa Polisi Tanzania hakuonyesha uchezaji wake wa kibabe kama anavyotambulika, hajawasumbua walinzi wa Simba unaweza sema alikuwa akiiogopa “Dani”.

 1. Mapinduzi Balama

Huyu ndiye mchezaji bora wa mchezo wa leo, sio kwamba alicheza vyema la hasha! Bali goli lake “la kideo” lilibadilisha kila kitu kwa Yanga na kusababisha kupata nguvu mpya.

Anapata alama 9.

 1. Haruna Niyonzima

Wengi hupenda kumuita fundi. Hakuwa na kazi kubwa bali kulainisha mipira migumu ya Makame, Tshishimbi kuwa rahisi kwa wachezaji wengine.

Anapata alama 6.

Akiba

-Metacha Mnata–hajatumika

-Vicent Andrew Dante– Anapata alama 5

-Feisal Salum Fei Toto— hajatumika

-Deus Kaseke– Anapata alama 4

-Mrisho Ngassa— hajatumika

-Patrick Sibomana— hajatumika

-Yikpe Gislein- Anapata alama 4.

Hiyo ndiyo tathmini ya kile ambacho nimekitazama na kubaini mchezo wa Simba dhidi ya Yanga katika ufanisi wa kazi zao dimbani.

Author: Bruce Amani