Telles wa Manchester United njia panda kuikabili West Bromwich Albion

Manchester United wana matumaini ya kumtumia beki wao mpya Alex Telles katika mchezo wa Ligi Kuu nchini England wa Jumamosi dhidi ya West Bromwich Albion licha ya kuwepo kwa taarifa kuwa mchezaji huyo amekutwa na dalili nyingine za Corona ikiwa ni mara ya pili.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 27 imeripotiwa kuwa amepimwa virusi vya Corona akiwa nyumbani kwao Brazil katika majukumu ya timu ya taifa na na kukutwa na maambukizi na atakosa mechi ya kesho Jumanne dhidi ya Uruguayi.

Itakumbukwa mara ya kwanza Telles kukutwa na maambukizi ya virusi vya Corona ilikuwa mwezi Octoba. Manchester United itafanya vipimo vyake baada ya nyota huyo kurudi kutoka kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Brazil ikiwa ni maandalizi ya kuelekea mechi za wikiendi hii. Telles alijiunga na United kutokea Porto kwa mkataba wa miaka minne.

Author: Asifiwe Mbembela