Tetesi – Higuain kusitisha mkataba wa AC Milan na kuhamia Chelsea

Mshambuliaji wa AC Milan Gonzalo Higuain “amefikia makubaliano binafsi“ na Chelsea ambayo inacheza ligi kuu nchini England kuelekea kukamilisha dili la kijiunga na klabu hiyo ya Stamford Bridge limeripoti gazeti la Italia la Gazetta Dello Sport.

Higuan alijiunga na Milan akitokea Juventus kwa mkopo wa msimu mzima huku kukiwa na kipengele cha kumnunua moja kwa moja endapo atafanya vyema ingawa amekuwa na wakati mgumu San Siro mpaka sasa amefunga goli 8 katika michuano yote.

Mshambuliaji huyo raia wa Argentina endapo atajiunga na Chelsea ataungana tena na kocha wake wa zamani Maurizio Sarri ambaye walikuwa pamoja katika klabu ya Napoli. “Chelsea imekubaliana na Higuain juu ya uhamisho wake” limeandika gazette hilo.

Higuain alikuwa katika kiwango bora sana alipokuwa chini ya Sarri katika msimu wa mwaka 2015/2016 ikishuhudiwa akivunja rekodi ya ufungaji bora akifikisha goli 36 huku akifanikiwa kufunga goli 91 katika miaka yake Napoli na baadae kuuzwa kwa pauni milioni 90 kwenda Juventus.

Higuain ni miongoni mwa washambuliaji waliocheza timu nyingi kubwa akiwa amewai kupita Real Madrid, Napoli, Juventus na River Plate misimu ya nyuma na sasa AC Milan. Mkurugenzi wa ufundi wa Milan Leonard ameonya kuwa mshambuliaji huyo hatatoka kwa sasa kwa sababu Higuan amekuwa na msimu mgumu tunahitaji kumrejesha kwanza katika hali yake.

“Hakuna mwenye shaka na uwezo wake wa kufunga lakini hali ikiendelea hivi hata sisi tutashindwa kumtetea. Alisema Leonardo ambaye aliongeza kwa kusema “tetesi za usajili hauwezi kuzipinga”

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends