Tetesi: Kocha Hitimana Thierry afutwa kazi Namungo FC

Kocha wa timu ya Namungo inayoshiriki Ligi Kuu nchini Tanzania kwa mara ya pili tangu ipande daraja inatajwa kumfuta kazi aliyekuwa kocha wao Hitimana Thierry kufuatia matokeo yasiyo ya kuridhisha.

Kocha huyo ambaye alikipandisha kikosi hicho Ligi Kuu Bara na msimu wake wa kwanza ndani ya Ligi aliweza kumaliza ndani ya tano bora kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Ikiwa imecheza jumla ya mechi 38 msimu wa 2019/20 ilishinda mechi 17, sare 13 na ilipoteza mechi nane huku ikikusanya jumla ya pointi 64 yakiwa ni miongoni mwa mafanikio makubwa kwa klabu hiyo ikiwa bado na kamba mguuni.

Msimu huu ikiwa inaiwakilisha nchi kimataifa katika Kombe la Shirikisho Afrika ipo nafasi ya tisa na pointi zake ni 14 baada ya kucheza mechi 10 jambo ambalo linaelezwa kuwa limewafanya viongozi wa Namungo kuamua kumfuta kazi.

Kibarua chake cha kwanza kimataifa kwa Namungo ni kati ya Novemba 27-29 ambapo itacheza na Al Rabita ya Sudan Kusini Uwanja wa Azam Complex.

Author: Asifiwe Mbembela