Tetesi za Mastaa bongo: Makambo, Djuma kutua Jangwani msimu 2021/22

Inaelezwa kuwa klabu ya Yanga imeanza mchakato wa kuzungumza na klabu ya Horoya inayoshiriki Ligi Kuu nchini Guinea kwa lengo la kuishawishi kumuachia mshambuliaji wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Heriter Makambo.

Makambo tangia asajiliwe na klabu ya Horoya mwishoni mwa msimu wa mwaka 2018/19 akitokea Yanga ameshindwa kutamba ndani ya klabu hiyo, kiasi cha Horoya kufikiria kumuuza mchezaji huyo katika dirisha hili linalotarajiwa kufunguliwa hivi karibuni.

Taarifa za kuaminika kutoka Yanga kimethibitisha kuwa, ni kweli wapo katika taratibu za kumrejesha mchezaji huyo ndani ya Yanga ambapo tayari wameshawasiliana na klabu ya Horoya juu ya kumrudisha mchezaji huyo, ambapo wameambiwa na uongozi wa klabu hiyo wanatakiwa kulipa kiasi tajwa cha pesa ili kumrudisha mshambuliaji huyo.

Hapo hapo Timu ya Wananchi Yanga, imebainika kuwa beki wa kulia wa AS Vita Club Djuma Shaban ni rasmi kutua klabuni hapo kwa kandarasi ya miaka miwili.

Djuma Shabani unakuwa ni usajili wa kwanza wa Yanga wa kimataifa ambapo klabu hiyo imelenga kukiboresha kikosi chao kuelekea msimu ujao ambapo timu hiyo inanafasi kubwa ya kushiriki michuano ya kimataifa.

Yanga chini ya Mwenyekiti msaidizi wa kamati ya usajili Eng. Hersi Said amesema kuwa timu hiyo itafanya usajili wa maana kwa ajili ya kufanya vizuri kwa msimu ujao katika mashindano yote ambayo watashiriki.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares