Tetesi za Mastaa Majuu:- Chelsea yaipiku Liverpool angani kupata saini ya Timo Werner, Brandon Williams aboreshewa mshahara Manchester United

Liverpool imesema hawatashindana na Chelsea juu ya kuwania saini ya mshambuliaji wa RB Leipzig Timo Werner 24, ambapo hivi sasa straika raia wa Ujerumani yuko mbioni kujiunga na The Blues.

Tottenham hawajui kitakachojiri juu ya hatima ya beki wake raia wa Ubeligiji Jan Vertonghen, 33, endapo kama atasalia mpaka mwishoni mwa msimu huu au ataondoka kabla.

Kiungo mkabaji wa Newcastle Matty Longstaff, 20, hajafanya mazoezi na wenzake wiki hii ambapo anahusishwa kwenda kujiunga na Udinese kwa ofa ‘bab kubwa’ ya £30,000 kwa wiki, kiungo huyo kandarasi yake inatamatika mwishoni mwa msimu huu.

Manchester United wanavutiwa kumpa mkataba mnono beki wake wa pembeni Brandon Williams, 19, baada ya mshambuliaji huyo kuwa katika msimu bora hivyo mshahara wake utapanda kutoka £4,000 mpaka ule ulioboreka zaidi.

Liverpool huenda wakatwaa ubingwa wa ligi kuu nchini England katika mchezo dhidi ya Everton baada ya michezo miwili kurudishwa nyuma.

Arsenal hawako tayari kuona mlinzi wa Scotland Kieran Tierney, 23, anaondoka klabuni hapo na kujiunga na Leicester City.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends