Tetesi za Mastaa Ulaya: Messi afikiria kubakia Camp Nou, Kocha mpya Barcelona amhitaji Georginio Wijnaldum

268

Inaelezwa kuwa staa wa Argentina Lionel Messi ameanza kufikiria kuendelea kusalia Barcelona baada ya kupewa ofa ya miaka miwili hivyo huweza akasalia ndani ya Camp Nou. Barca imefanya kikao cha ndani na babake Messi anayefahamika kwa jina la Jorge kwa ajili ya kujadili hatima ya staa huyo baada ya kuhusishwa kuondoka na kujiunga na matajiri wa Manchester City.

Rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu alisema hawezi kuzungumza juu ya bei ya staa huyo maana bei yake ndio hitimisho timu inayomhitaji lazima itoe pesa. Ili uweze kumng’oa Messi Barcelona ni lazima uwe na fedha kama Euro milioni 100 (pauni milioni 88.8).

Manchester United wameingilia kati mbio za kuwania saini ya kiungo mshambuliaji wa Bayern Munich Thiago Alcantara, 29, kufuatia Liverpool ambao waliokuwa wanapewa nafasi ya kumchukua kusuasua.

Mlinda mlango wa England Dean Henderson, 23, ameionya klabu yake ya Manchester United kuwa ataondoka klabuni hapo endapo atakuwa kipa namba mbili nyuma ya Mhispania David de Gea licha ya kuongeza mkataba mpya ndani ya Old Trafford.

Kocha mpya wa Barcelona Ronald Koeman anahitaji klabu hiyo kufanya usajili wa kiungo mkabaji wa Liverpool na Uholanzi Georginio Wijnaldum, 29.

Newcastle wanavutiwa kumsajili winga wa AFC Bournemouth na Scotland Ryan Fraser, 26,  kama mchezaji huru baada ya kandarasi yake na Bournemouth kumalizika mwezi Juni.

Paris St-Germain wamefuta uwezekano wa kumsajili kiungo mkabaji wa Arsenal na raia wa Ufaransa Matteo Guendouzi, 21.

Author: Asifiwe Mbembela