Tetesi za Mastaa Ulaya: Aguero ageuka nuru Ulaya, Everton, Chelsea ndani, Ramos kujipiga kitanzi Madrid

Everton imejiunga na Chelsea, Leeds United, Tottenham, Barcelona na Inter Milan katika kuwania ya mshambuliaji wa Manchester City Sergio Kun Aguero, 32, ambaye ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu baada ya kandarasi yake kumalizika.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Misri Mohamed Salah amesema Liverpool hawajazungumza lolote naye juu ya mkataba mpya wa kuendelea kusalia klabuni hapo, kandarasi ya Salah, 28, inafikia ukomo 2023.

Arsenal wanaamini wanaweza kufanya uhamisho wa kiungo mkabaji wa Mali Brighton Yves Bissouma 24 ambaye yuko sokoni kwa dau la pauni milioni 30.

Beki wa kati wa Real Madrid Sergio Ramos, 35, bado anamatumaini ya kuendelea kukitumikia kikosi hicho kwa kandarasi ya ziada ya miaka miwili, licha ya klabu hiyo kumpa mwaka mmoja.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares