Tetesi za Mastaa Ulaya: Arsenal kumuuza Saka na kumbeba Martin Odegaard wa Real Madrid

Kiungo mshambuliaji wa Manchester United Juan Mata, 32, anakaribia kusaini mkataba mpya wa kuendelea kukitumikia kikosi hicho, inatajwa amepewa ofa ya mwaka mmoja.

Mtendaji Mkuu wa kandanda ndani ya klabu ya Borrusia Dortmund Sebastian Kehl amekiri kuwa itafika muda ambao hawataweza kumzuia mshambuliaji wa kimataifa wa Norwei Erling Braut Haaland, 20.

Hata hivyo, Haaland anawindwa na Manchester City, Barcelona na Real Madrid kutokana na ubora mkubwa ambao ameonyesha ndani ya Salzburg, Dortmund na Norwei.

Washika mtutu wa London, klabu ya Arsenal inafikiria kumuuza winga wao raia wa England Bukayo Saka, 19, ili kupata fedha za kumsainisha kiungo mshambuliaji wa Real Madrid ambaye anakipiga klabuni hapo kwa mkopo Martin Odegaard, 22.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares