Tetesi za Mastaa Ulaya; Arsenal wanahitaji kuvunja mkataba wa Ozil

Arsenal wanahitaji kuvunja mkataba wa kiungo mshambuliaji wao na Ujerumani Mesut Ozil, 31, kabla ya dirisha dogo la usajili la mwezi Januari.

Manchester City inaendelea na mazungumzo na kiungo wao wa kimataifa wa Ubeligiji Kelvin de Brune, 29, wanataka kumpa mkataba wa miaka mitano.

Manchester United watajaribu kumsaini beki wa kati wa RB Leipzig Dayot Upamecano na Ufaransa katika majira ya usajili wa dirisha dogo la Januari, pauni milioni 36 zinahitajika kumng’oa klabuni hapo.

Winga wa Uholanzi na Lyon Memphis Depay, 26, amesema baadhi ya sheria ndizo zilizomkwamisha kutua katika klabu ya Barcelona katika dirisha kubwa la usajili.

Kiungo kisheti wa Ufaransa na Lyon Houssem Aouar, 22, amesema hakukatishwa tamaa na kushindwa kujiunga na Arsenal katika dirisha kubwa la usajili.

Author: Bruce Amani