Tetesi za Mastaa Ulaya: Arsenal yakomalia dili la Dembele, Mauro Icardi kusalia PSG

Bayern Munich wamepanga kutoa ofa ya mlinzi wa Kifaransa Lucas Hernandez, 24, kwenda Manchester City ili iwe sehemu ya ushawishi wa kumnasa winga wa klabu hiyo Leroy Sane, 24. Sane amekuwa akihusishwa kujiunga na miamba ya Ujerumani kwa muda sasa licha la dau ambalo wapo tayari kutoa kuwa dogo.

Mshambuliaji wa Argentina Mauro Icardi, 27, amekusudia kusalia Paris St-Germain moja kwa moja baada ya dili la £51.2m ambalo PSG wako tayari kutoa kukubaliwa na klabu mama ya Inter Milan.

AC Milan wanavutiwa kumsajili kiungo wa Burnley na raia wa Jamhuri ya watu wa Ireland Jeff Hendrick, 28, kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu.

Wakala wa mlinzi wa pembeni wa Borussia Dortmund Achraf Hakimi, 21, ambaye yuko kwa mkopo klabuni hapo kutokea Real Madrid amesema kipaumbele cha beki huyo ni kucheza katika klabu yake mama ya Real Madrid lakini hana haraka ya kurudi Hispania kwa sasa.

Arsenal wamekamilisha usajili wa kinda mwenye asili ya Rwanda ambaye anauwezo wa kuichezea pia Norwei George Smith, 19.

Katika kuimarisha kikosi chake kocha wa Arsenal Mikel Arteta amefufua hitaji lake juu ya kuwania saini ya strika matata wa Lyon na Ufaransa Moussa Dembele, 23, tayari amefanya mazungumzo ya awali na wawakilishi wake.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends