Tetesi za Mastaa Ulaya: Arsenal yamweka sokoni Aubameyang, Harry Kane, Levy ngoma ngumu Tottenham

Arsenal wako tayari kumuachia mshambuliaji wake raia wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang 32, endapo ataonyesha nia ya kuondoka klabuni hapo, klabu ya Paris St-Germain na Fc Barcelona imekuwa ikiwani saini yake.

Inaonyesha hata baadhi ya mashabiki wako tayari kumuachia nahodha wao chini ya kocha mwenye hofu kwa hivi sasa Mikel Arteta kufuatia kupoteza mechi mbili za awali za EPL.

Kocha wa zamani wa Chelsea na Inter Milan Antonio Conte anafikiria kujiunga na Arsenal endapo dili la Arteta klabuni hapo litaota mbawa kufuatia matokeo mabovu.

Mwenyekiti wa klabu ya Tottenham Daniel Levy amesema kuwa hatashusha thamani ya Harry Kane 28, ya pauni milioni 150, licha ya kukumbwa na shinikizo kutoka kwa nahodha huyo wa England kwenda kwa Manchester City.

Wolves wamekataa ofa ya Tottenham Hotspur ya kuhitaji huduma ya kumsajili winga wa Adama Traore 25 kwa mkopo.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends