Tetesi za Mastaa Ulaya: Arsenal yatimba kwa Locatelli, Paul Pogba kutua PSG

Kiungo mshambuliaji wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba 28, anawindwa na klabu ya Paris St-Germain inayoshiriki Ligi Kuu Ufaransa Ligue 1, takribani pauni milioni 50 inaandaliwa kwa Pogba.

 

Bado klabu ya PSG haijafanya mazungumzo yoyote na Manchester United kuhusu nyota huyo wa zamani wa Juventus.

 

Uhamisho wa beki wa kati wa Real Madrid na Ufaransa Raphael Varane, 28, uko mbioni kukamilika, inatajwa siku chache utatangazwa.

 

Klabu ya Arsenal imeandaa kiasi cha pauni milioni 34 kwa ajili ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa Sassuolo na Italia Manuel Locatelli, 23.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares