Tetesi za Mastaa Ulaya: Baba mzazi wa Messi atimba Barcelona kumalizana na wakubwa

Manchester United bado wanahitaji kumsajili winga wa kimataifa wa England na Borussia Dortmund Jadon Sancho, 21, licha ya msimu uliopita wa kiangazi kushindikana kwa dili hilo.

Baba mzazi wa nyota wa Argentina na Barcelona Jorge Messi amekutana na Rais wa klabu hiyo Joan Laporta kwa lengo la kujadili hatima ya mtoto wake Lionel Messi, 33, ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu.

Wananusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Chelsea wapo tayari kusikiliza ofa yoyote kwa mshambuliaji wao Tammy Abraham, 23, baada ya mchezaji huyo kupoteza nafasi ya kuanza tangia kuondoka klabuni hapo kocha Frank Lampard.

Kocha wa Leicester City Brendan Rodgers, ambaye alikuwa anahusishwa kujiunga na Tottenham amesema ana furaha kuendelea kukitumikia kikosi cha Mbweha hao.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares