Tetesi za Mastaa Ulaya: Barcelona kufyeka majina ya mastaa mzigo, Messi, Ter Stegen wako salama, Pogba kizungumkuti Manchester United

Wakala wa Paul Pogba Mino Raiola ameanza mazungumzo ya kukamilisha dili la kumhamisha bosi wake kwenda Juventus katika dirisha kubwa la usajili msimu huu, hata hivyo Juventus watakumbana na ugumu kwani Real Madrid, na Paris Saint-Germain wanahitaji huduma ya kiungo huyo.

Miamba ya Ujerumani Bayern Munich huenda ikaingia kwenye mbio za kunasa saini ya winga wa Borrusia Dortmund Jadon Sancho, 20, ambaye anawindwa na kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer.

Barcelona watafungua milango kwa wachezaji wake takribani sita kwenda kwingineko katika kipindi cha usajili majira ya kiangazi ili kupunguza gharama za kuendesha timu hiyo baada ya kuathirika za Corona.

Hata hivyo panga la Barcelona halitawagusa wachezaji hawa kutokana na umuhimu mkubwa walionao kwenye kikosi hicho mlinda mlango wa Kijerumani Marc-Andre ter Stegen, 28, mshambuliaji wa Argentina striker Lionel Messi, 32, na kiungo wa Uholanzi Frenkie de Jong, 23.

Mlinzi wa kati wa Barcelona Samuel Umtiti, 26, anaweza kufanyika chambo cha kuishawishi Inter Milan kumwachia strika wao raia wa Argentina Lautaro Martinez, 22.

Wakala wa mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero, 31, amekanusha taarifa zinazomhusisha bosi wake kutaka kuihama timu hiyo mwishoni mwa msimu huu na kurudi kwao Argentina.

Winga wa Chelsea Willian, 31, amesema klabu yake imekataa kumpatia kandarasi ya miaka mitatu ili aendelee kuitumikia, hali hiyo imemuacha njia panda.

Southampton watalazimika kuwauza mastaa wake kama Danny Ings, 27, Nathan Redmond, 26, na James Ward-Prowse, 25, kama klabu haitapa mnunuzi wa hisa zaidi ya asilimia 80.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends