Tetesi za Mastaa Ulaya: Barcelona yavamia England waisaka saini ya Rudiger, Shkodran Mustafi wa Arsenal

Manchester United wamebakia kwenye matamanio ya kumsajili winga wa Borrusia Dortmund na England Jadon Sancho, 20, ambapo mpango wa hivi sasa ni kukamilisha uhamisho wake kabla ya kuanza kwa michuano ya Ulaya mwaka ujao.

Paris St-Germain watatuma ofa kwenda kwa Real Madrid juu ya kuhitaji huduma ya mlinzi kitasa na nahodha wa kikosi hicho Sergio Ramos, 34, ambaye anamaliza mkataba wake.

Everton na Tottenham Hotspur wanavutiwa na fowadi wa Napoli na Poland Arkadiusz Milik mwenye umri wa miaka 26 ambapo anaweza kupatikana kwa dau la pauni milioni 10 mwezi Januari.

Celtic wamenuia kumvuta kipa wa Manchester United ambaye amepoteza nafasi ya kuanza Dean Henderson, 23, kwa mkopo wa nusu msimu.

Barcelona wanamtumia beki wa Arsenal na Ujerumani Shkodran Mustafi, 28, kama chaguo la pili endapo watashindwa kuinasa saini ya beki wa Chelsea Antonio Rudiger 27 ambaye ndiye chaguo la kwanza kwa klabu hiyo Hispania.

Author: Bruce Amani