Tetesi za Mastaa Ulaya: Bei ya Grealish wa Aston Villa yawakimbiza United na City, Ziyech Bye Bye Chelsea

Kocha wa kimataifa wa Italia na aliyekuwa Juventus Andrea Pirlo pamoja na aliyekuwa kocha wa Inter Milan Antonio Conte wameingia kwenye vita ya kuwania nafasi ya kocha ndani ya Everton kufuatia Bosi wa timu hiyo Farhad Moshiri kuwa bila kocha.
Kiungo wa Aston Villa na England Jack Grealish, 25, huenda akaendelea kubakia Villa Park msimu huu kufuatia klabu ya Manchester United na Manchester City kutokuwa tayari kutoa kitita kirefu cha pauni milioni 130.
Chelsea haijaweka wazi kama wana nia ya kumuachia winga wa Morroco Hakimi Ziyech, 28, ambapo klabu ya AC Milan na Napoli zimeonyesha nia ya kumsajili winga huyo wa zamani wa Ajax ya Uholanzi.
AC Milan wameongea na Chelsea kuhusu hatima ya beki wa kati Fikayo Tomori, 23, ambapo wako tayari kulipa pauni milioni 28.5 zilizopo kwenye mkataba wake na the blues.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares