Tetesi za Mastaa Ulaya: Chelsea kumbakisha Aguero England, Man United, Liverpool vitani kwa Konate

Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina Sergio Kun Aguero, 32, anahitaji kuendelea kubakia Ligi Kuu nchini England ili kuendelea kujiwekea rekodi ya magoli, timu ya Chelsea imeonyesha nia ya kumsajili staa huyo.

Aguero yuko tayari hata kutocheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao ilimradi abakie England kucheza EPL – Chelsea na Tottenham zimeonyesha nia ya kumhitaji.

Manchester United wameungana na Liverpool kuwania saini ya mlinzi wa kati wa RB Leipzig Ibrahima Konate 21 ambaye ni raia wa Ufaransa, yuko sokoni kwa dau la pauni milioni 34.

West Ham watajaribu kumsajili moja kwa moja kiungo mshambuliaji wa Manchester United Jesse Lingard, 28, ambaye yuko klabuni hapo kwa mkopo baada ya kuonyesha kandanda safi tangia ajiunge nayo kwenye dirisha dogo la usajili.

Arsenal wanafikiria kumtoa mshambuliaji wao wa kati raia wa Ufaransa Alexandre Lacazette, 29, klabu ya Inter Milan, Roma na Sevilla zimeonyesha nia.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares