Tetesi za Mastaa Ulaya: Chelsea wagonga ukuta kwa Haaland, macho kwa Sergio Aguero wa Man City

Majogoo wa Jiji la Merseyside Liverpoolol wanakutana na wakati mgumu wa kumbakisha nyota wa kimataifa wa Misri Mohamed Salah, 28, hasa baada ya mchezaji huyo kuonyesha matamanio ya kuondoka klabuni hapo.

Manchester United na Chelsea zote zimejiegesha kufanikisha usajili wa winga wa Hispania na klabu ya Real Madrid Lucas Vazquez, 29.

Chelsea wanamuangalia mshambuliaji wa Manchester City na Argentina Sergio Kun Aguero 32, kama mbadala wa dili la Erling Braut Haaland 20 ambaye kwa sasa anahusishwa kujiunga na miamba ya soka mbalimbali Ulaya kama Manchester City, Real Madrid, Barcelona na PSG.

Real Madrid wako tayari kumuachia kiungo mshambuliaji Martin Odegaard ilikukuza pato la kwenda kuwania saini ya mshambuliaji wa Borrusia Dortmund Haaland, Arsenal wanaweza wakawa wamerahisishiwa kazi ya kumsajili moja kwa moja akimaliza muda wa mkataba.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares