Tetesi za Mastaa Ulaya: Chelsea waibukia kwa straika anayewindwa na Liverpool Timo Werner, David Luiz kupewa kandarasi mpya Arsenal

Chelsea wameanza kufikiria uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa RB Leipzig anayewindwa vikali na Liverpool Timo Werner, 24, endapo tu straika huyo ataonyesha nia ya kuondoka klabuni hapo.

Mshindi mara sita wa Ballon d’Or Lionel Messi, 32, ataendelea kuwa sehemu ya kikosi cha Fc Barcelona kwa msimu ujao baada ya kipengele kilichokuwa kinamruhusu kuondoka huru kuisha muda wake msimu huu.

Real Madrid wamesitisha zoezi la kumsajili winga wa Chelsea Willian, 31, kama mchezaji huru, kandarasi ya staaa huyo wa Brazil ina malizika mwishoni mwa msimu huu.

Manchester United watalazimika kulipa £10.5m kwa kumuongezea kandarasi ya mkopo ya miezi sita mshambuliaji wa Nigeria Odion Ighalo, 30, £6 zinaenda katika klabu ya Shanghai Shenhua kama malipo na £130, 000 kama mshahara wake kwa wiki.

Arsenal wako tayari kuanza mazungumzo na beki wao David Luiz, 33, juu ya kujadili mkataba mpya wa mwaka mmoja wenye thamani ya £130,000 kwa wiki.

Kocha mkuu wa kikosi cha England Gareth Southgate hata hudhuria mechi hata moja ligi ikirejea ya EPL baada ya kuhisi kutokuwa na umuhimu wa kuwepo katika awamu hii.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends