Tetesi za Mastaa Ulaya: Chelsea wapunguza dau la kumuuza Victor Moses, Sane aandaliwa jezi Bayern Munich

Bayern Munich imemtengea winga wa Manchester City na Ujerumani Leroy Sane, 24, jezi namba 10 kwa msimu ujao.

Chelsea watapunguza bei ya mlinzi wa Kinigeria Victor Moses ambaye Inter Milan wamegoma kutoa £10.75m.

Wakala wa Jorginho amesema bosi wake ana furaha ya kuendelea kusalia The Blues ambapo amethibitisha kuwa Juventus hawajafanya nae mazungumzo yoyote.

Liverpool wako tayari kuwauza wachezaji wake watatu ili kuongezea dau la kumnunua mshambuliaji wa RB Leipzig Timo Werner ambaye dau lake linakadiriwa kufikia £52.

Manchester United wanahitaji kumbakiza mshambuliaji wa Shanghai Shenhua Odion Ighalo, 30, lakini hawana pupa ya kumsajili kwa sababu mshambuliaji wao Marcus Rashford amepona majeruhi yake.

Arsenal wanafikiria kufanya biashara ya mabadiliko ya wachezaji, The Gunners wamekusudia kumtoa straika Alexandre Lacazette, 28, na kiungo mshambuliaji wa Atletico Madrid Thomas Lemar, 24 atakuja Emirates.

Neymar, 28, hataondoka ndani ya Paris St-Germain na kujiunga na miamba ya Catalunya FC Barcelona kutokana na athari kubwa za kiuchumi ambazo vilabu vimekubwa na kadhii hiyo iliyo sababishwa na Covid-19.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends