Tetesi za Mastaa Ulaya: Chelsea yajitosa kwa mlinzi wa Bayern Munich Niklas Sule

Bosi wa zamani wa Leicester na Watford Nigel Pearson anakaribia kuichukua timu ya Bristol City kufuatia mazungumzo mazuri na klabu hiyo inayoshiriki Ligi daraja la kwanza England.

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norwei Erling Braut Haaland 20 amesema anahitaji pauni milioni 78 kutoka kwenye klabu ambayo inahitaji huduma yake.

Manchester United wanafikiria uwezekano wa kumsajili mlinda mlango wa AC Milan na Italia Gianluigi Donnarumma, 21 ambaye amekuwa kwenye kiwango bora msimu huu.

Chelsea inaelezwa kuwa imeanza mazungumzo na klabu ya Bayern Munich juu ya kufanya uhamisho wa beki wa kati wa Ujerumani Niklas Sule, 25 Euro milioni 30 zinahitajika.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares