Tetesi za Mastaa Ulaya: Chelsea yapanga kumrejesha Hazard, Dembele kutimkia Liverpool

Chelsea imeanzisha mazungumzo ya kumsajili tena kiungo mchezeshaji wa kimataifa wa Ubeligiji Eden Hazard, 30, hata hivyo watatakiwa kumuachia Reece James, 21, kwenda Real Madrid.

Liverpool wako karibu kumtazama winga wa kimataifa wa Ufaransa na Fc Barcelona Ousmane Dembele, 24, ambaye hajacheza mechi yoyote tangia michuano ya Euro 2020 kutokana na majeruhi.
Kocha wa zamani wa Borussia Dortmund Lucien Favre, 63, na aliyekuwa kocha wa Chelsea Frank Lampard, 43, ni miongoni mwa majina ambayo yanatajwa kuchukua mikoba ya kukinoa kikosi cha Newcastle United kupitia mambwenyenye wapya.
Mshambuliaji wa Arsenal na Ufaransa Alexandre Lacazette, 30, hana mpango ya kuongeza mkataba mpya wa kuendelea kukitumikia kikosi hicho, baada ya mkataba wake kumalizika klabuni hapo.
Kiungo mshambuliaji wa Wales Aaron Ramsey, 30, bado anaamini kuwa anaweza kufanikiwa katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu ambao umebakia kwenye kandarasi yake.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends