Tetesi za Mastaa Ulaya: Chiellini mlinzi wa Juventus akubali uwezo wa Ramos wa Real Madrid, Mbappe yupo yupo sana PSG

264

Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 21, hatalazimisha kuondoka Paris St-Germain katika dirisha kubwa la usajili msimu huu kutokana na vilabu vingi kukumbwa na anguko la uchumi lililochagizwa na Covid-19, hivyo staa huyo ataendelea kuwa sehemu ya kikosi cha mabwenyenye hao kutoka Ligue 1.

Juventus huenda wakamrudisha kiungo mshambuliaji wa Manchester United Paul Pogba, 27. Katika dili hilo wanafikiria kumwachia kiungo Adrien Rabiot, 25, kwenda United kama sehemu ya kupunguza gharama za usajili.

Licha ya utayari huo wa Juventus bado watakumbana na ushindani kutoka kwa Real Madrid ambapo Zinedine Zidane siku zote amekuwa akihusudu kufanya kazi na Paul Labile Pogba.

Barcelona na Real Madrid wanavutiwa kumsajili winga wa Borrusia Dortmund Jadon Sancho, 20, licha ya United kuwa timu inayotazamiwa zaidi kumnyaka winga huyo raia wa England.

Wakati huo huo Chelsea watapokea £48.5m kutoka kwa Atletico Madrid kwa ajili ya kiungo wa Kihispania Alvaro Morata, 27, majira haya, ambapo wamekusudia kupeleka donge hilo kwa winga wa Borrusia Dortmund Jadon Sancho.

Staa wa Barcelona Lionel Messi amesifia kiwango cha mshambuliaji wa Argentina ambaye ni raia mwenza na Inter Milan Lautaro Martinez, 22, sifa hizo zinakuja kipindi hiki ambacho straika huyo anahusishwa kutua na dimba la Camp Nou.

Mlinzi mkongwe wa Juventus na Italia Giorgio Chiellini amesema beki kitasa wa Real Madrid Sergio Ramos alitumia mbinu za kivita (masterstroke) dhidi ya Mohammed Salah, mbinu iliyopelekea majeruhi kwa staa huyo wa Liverpool katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Uefa msimu wa 2018.

Author: Bruce Amani