Tetesi za Mastaa Ulaya: de Gea yupo sana Man United, Chelsea yamtaka Achraf Hakimi na Haaland

Chelsea inahitaji huduma ya beki wa kulia wa Inter Milan na timu ya taifa ya Morroco Achraf Hakimi, 22, mchezaji ambaye Paris St-Germain wanahitaji kumsajili pia. Wakati huo huo The Blues wametenga kitita kirefu kwa strika wa Dortmund Braut Haaland.

Kocha wa zamani wa Liverpool na Newcastle United anatajwa kuchukua mikoba ya Carlo Ancelotti katika klabu ya Everton.

Barcelona wamemweka winga wa Manchester City na England Raheem Sterling 26, tayari kumsajili endapo winga wa Kifaransa Ousmane Dembele 24, ataamua kuondoka klabuni hapo kulingana na tetesi zinazomhusisha.

Licha ya kukumbwa na ukosoaji mwingi, mlinda mlango wa Hispania David de Gea, 30, anatarajia kuendelea kusalia ndani ya Manchester United katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi ya usajili.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares