Tetesi za Mastaa Ulaya: Dortmund yapunguza bei ya Sancho kwenda Man United, Conte aikaushia Spurs

Klabu ya Borussia Dortmund inayoshiriki Ligi Kuu ya kandanda Ujerumani -Bundesliga imeiambia Manchester United kuwa itawagharimu kiasi cha pauni milioni 81.5 kumpata winga wa England Jadon Sancho 21, badala ya pauni 100m ya msimu uliopita.
Endapo dili hilo litakamilika, basi Manchester City itavuna kiasi cha pauni milioni 11 kama faida ya kumlea winga Sancho klabuni Etihad kabla ya kuuzwa Dortmund.
Tottenham wameamishia matamanio ya kumsajili kocha wa Ajax Erik ten Hag, 51, kufuatia dili la kumpata kocha wa zamani wa Inter Milan Antonio Conte kuota mbawa.
West Ham wana uhakika kuwa kocha David Moyes, 58, ataongeza mkataba mpya licha ya kuhusishwa kurejea tena katika klabu ya Everton kufuatia kocha Carlo Ancelotti kutimkia Real Madrid.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares