Tetesi za Mastaa Ulaya: Euro milioni 200 kumtoa Haaland Dortmund, Arsenal yajikwaa kwa Odegaard

Mtendaji Mkuu wa klabu ya Paris St-Germain Nasser Al-Khelaifi amesema hawako tayari kumuachia winga hatari wa Ufaransa Kylian Mbappe 22, licha ya kuhusishwa kujiunga na klabu nyingine Ulaya.
Imebainika kuwa timu inayohitaji huduma ya mshambuliaji wa kimataifa wa Norwei na klabu ya Borrusia Dortmund Erling Braut Haaland 20, itatoa kiasi cha pauni milioni 171.8.
Klabu ya Aston Villa imepanga kufanya usajili wa kiungo wa Southamption na England James Ward-Prowse, 26, siku chache baada ya kuvunja rekodi ya kumsajili kiungo Emiliano Buendia.
Baada ya kukosa huduma ya Buendia, Arsenal imeingia sokoni kusaka nafasi ya kiungo mshambuliaji ambapo jina la kiungo wa Real Madrid Martin Odegaard 22, anatajwa kubakia ndani ya viunga vya Emirates.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares