Tetesi za Mastaa Ulaya; Everton, West Ham zahusishwa kwa Perisic, Newcastle wasaka kocha

Everton na West Ham ni miongoni mwa timu ambazo zinawania saini ya winga wa kimataifa wa Croatia na Inter Milan Ivan Perisic, 32.

Newcastle United watalazimika kutoa fedha nzito kumshawishi kocha wa Ajax Erik ten Hag ambaye amekuwa akihusishwa kujiunga nayo kuchukua mikoba ya Steve Bruce.

Kiungo wa Angers ya Ufaransa Angelo Fulgini, 25, ameanza kuwindwa na klabu za Ligi Kuu England baada ya kuonyesha kiwango kizuri dhidi ya Paris St-Germain.

Kocha wa West Ham United David Moyes amesema timu itakayohitaji huduma ya kumsajili kiungo mkabaji Declan Rice watalazimika kutoa kiasi cha pauni milioni 100.

Kiungo wa Ufaransa Tanguy Ndombele, 24, amesema kuwa amekutana na Mwenyekiti wake Daniel Levy kuangalia uwezekano wa kubakia Tottenham Hotspur.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends