Tetesi za Mastaa Ulaya: Ferguson awekwa kando kumpata mrithi wa Solskjaer Man United, Ziyech awindwa na Barcelona

Manchester United wako tayari kuachana na mpango wa kumchukua kocha wa muda wa kukinoa kikosi endapo watampa kocha Mauricio Pochettino wa Paris St-Germain.

Kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane, ni jina lingine ambalo linatajwa kuwa linaweza kutua viunga vya psg endapo Mauricio Pochettino atakubali kujiunga na Manchester United Old Trafford.

Imewekwa wazi kuwa kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson, ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ndani ya United hatahusika kwenye usajili wa kocha mpya klabuni hapo, tofauti na baadhi ya tetesi.

Liverpool na Barcelona zinavutiwa kumsajili kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Marekani Chelsea Christian Pulisic, 23.

Barcelona wanaangalia uwezekano wa kumsajili winga wa Chelsea na timu ya taifa ya Morocco Hakim Ziyech, 28, pamoja na Timo Werner 25, raia wa Ujerumani kama mbadala wa Raheem Sterling 26.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends