Tetesi za Mastaa Ulaya: Grealish, Kane waitesa Man City, Zaha aombwa kubaki Crystal Palace

Mshambuliaji wa kimataifa wa England na Tottenham Hotspur Harry Kane 27, na kiungo mshambuliaji wa Aston Villa Jack Grealish 25, wameendelea kuwindwa na Manchester City kwa ajili ya usajili licha ya ugumu ambao klabu zao zimekuwa zikiuweka.

 

Grealish ambaye ni nahodha wa Villa anategemewa kumwaga wino wa miaka mingi zaidi kuendelea kusalia klabuni hapo.

 

Real Madrid watalazimika kuendelea kumtumia winga wa Wales Gareth Bale 31, kufuatia kutopokea

ofa yoyote kwa mchezaji huyo ambaye msimu uliopita alikuwa Spurs kwa mkopo.

 

Arsenal imefikia makubaliano na na Brighton ya kumsajili beki wa kati wa timu hiyo Ben White 23, ambaye thamani yake ni pauni milioni 50.

 

Crystal Palace wanamatumaini ya kumbakiza kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast Wilfred Zaha, 28, kutokana na usajili wa kocha mpya Patrick Vieira.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares